Mkali wa ‘Mboga Saba’, Mr Blue ameonesha kuwa na wasiwasi na kinachoendelea katika muziki wa kizazi kipya kwa sasa kwa kukimbizana na mabadiliko na ukuaji wake.

Ingawa rapa huyo amesifia mabadiliko hayo kuwa wasanii wa sasa wanafanya vizuri kwa kulinganisha na hali ilivyokuwa mwazo, amesema huenda muziki wa Bongo Flava asilia ukapotea.

“Kwa upande wangu naona muziki umekuwa sana, yaani umebadilika. Wasanii kwa sasa wanafanya vizuri sana ukilinganisha na zamani wakati tunaanza. Sasa hivi kidogo watu wamebadilika japo kuwa pia nina wasiwasi kwamba unaweza ukapotea kwa sababu wasanii wamekuwa wakienda na wakati. Kwahiyo wanakuwa wanakimbia kwenye ule uasilia wa muziki,” Blue anakaririwa na Dizzimonline.

Hata hivyo, amesema kuwa mabadiliko hayo sio kitu kibaya kwakuwa hata Marekani wameanza kuupoteza muziki wa hip hop asilia na badala yake wamejikita katika kufanya muziki wa biashara.

?Live: Yanayojiri Bungeni Serikali ikiwasilisha wa Bajeti Kuu 2017/2018
Birdman amtamani 50 Cent, aahidi kumrejeshea ukwasi wa ‘Get Rich Or Die Tying’