Mrembo mmoja wa nchini Kenya aliefahamika kwa jina la Cleo Maina ameaga dunia katika mazingira ya kushtusha baada ya kuchapisha ujumbe unaotia wasiwasi katika mtandao wake wa Twitter Disemba 29, 2021.

Cleo alichapisha ujumbe wa kuzua wasiwasi kwenye ukurasa wake wa Twitter ulionyesha kuwa mambo hayakuwa sawa uliosomeka “Part of the Journey, is the End.. akimaanisha Sehemu ya safari ni mwisho…,” aliandika.

Siku na chache baadaye, kifo chake kilitangazwa na mwanahabari Oliver Mathenge ambaye alikuwa rafiki yake wa karibu.

Mathenge alimuelezea marehemu kama mtu mwema ambaye walifurahia wakati wao pamoja. “Uliona bora kwangu kila wakati hata nisingeweza! Kila mara ukiniita nje ninapopotea! Ulisherehekea ushindi wangu kama ni wako mwenyewe. Tulishiriki nyakati za ajabu. Wakati mwingine tulilia. Mtu wa karibu sana ambaye nimelazimika Dada mmoja. Nitakusherehekea kila wakati, Cleo,” aliomboleza, katika mtandao wake wa Twitter.

Oliver akiwa na Cleo enzi za uhai wake.

Wakenya walijitokeza kwa wingi kwenye Twitter kumuomboleza Cleo wakimtaja kama mtu aliyekuwa mchangamfu na mwingi wa furaha.

@exclusivedeejay aliandika, “Kuniangalia hata sikustahili na upendo wake aliutoa kwa moyo wote. Nitakukumbuka sana Cleo na drives zote tulizokuwa tukichukua bila mpangilio, tende za matumbo, Keki ungeoka na kunitumia. na masomo ya Kihispania uliyojaribu kunipa.Lala salama mpenzi.”

Exclusivedeejay akiwa na Cleo enzi za uhai wake.

Clifford Biko aliomboleza: “Nilifanya kazi katika mradi na wewe muda mfupi uliopita na lazima niseme jicho lako kwa maelezo na hamu ya kujua zaidi kila wakati ilikuwa ya kupendeza. Ulikuwa na sauti nzuri. Hakika Mbingu imepata Malaika. Pumzika vizuri.”

Hata hivyo haikuweza kufahamika ni nini chanzo cha kifo chake Cleo.

Hata hivyo imekua ikitokea kwa watu maarufu duniani kujitabiria vifo vyao ikiwemo wasanii kwa kuimba nyimbo zinazoashiria kuitwa mbinguni, pia waigizaji ambao wamekua wakiigiza kufariki na wakafariki kweli, wakiwemo watu walioandika katika mitandao yao ya kijamii na wakafariki kweli.

Hakuna  ajuaye siku wala saa Kifo kitakapotokea ni fumbo kubwa katika maisha ya mwanadamu.

Otile Brown  namba moja youtube Kenya
Mgonjwa ashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuiba gari la wagonjwa