Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, imekiandikia barua chama cha ACT – Wazalendo kujieleza na kutoa ufafanuzi kuhusu mazungumzo ya Mwenyekiti wao Zitto Kabwe na Ubalozi wa Uingereza Tanzania.

ACT wametakiwa kuwasilisha maelezo hayo ndani ya siku saba, kuanzia tarehe 12 Juni 2020 hadi Juni 19 saa 9:30 mchana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahozi, imeeleza kuwa kati ya tarehe 8 hadi 12 juni 2020, Zitto alifanya mazungumzo na Sarah Cooke, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam.

Taarifa hiyo inafafanua kuwa ACT – Wazalendo wanapaswa kujieleza kwakuwa hatua yake hiyo imekwenda kinyume na sheria ya vyama vya siasa, inayokataza mtu asiye Raia wa Tanzania kufanya vikao na viongozi wa vyama vya siasa.

Burundi: Mahakama ya yaagiza kuapishwa kwa rais mteule mapema
Tanzania, Kenya bendera zapepea nusu mlingoti kuomboleza kifo cha Nkurunziza