Kiungo Mshambuliaji wa Singida Big Stars James Msuva amesema wapo tayari kwa mchezo wa Mzunguuko wanne wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Geita Gold FC.

Singida big Stars kesho kujatano (Septemba 21) itacheza ugenini jijini Mwanza, ikiwa mara ya kwanza kucheza nje ya Uwanja wao wa nyumbani wa Liti mkiani Singida.

Msuva amesema wamejiandaa vyema kuipa matokeo chanya timu yao huku akiahidi safu yao ya ushambuliaji kufunga na kumaliza tatizo la uhaba wa mabao.

“Hakuna mchezo mwepesi lakini kwa maandalizi yetu tuliyofanya tunaamini tunaweza kupata ushindi japo mengine tunamuachia mwenyezi Mungu,”

“Sisi kama washambuliaji tunahitaji kufunga na hilo tumekaa na kulifanyia kazi naamini kuna kitu kimetengenezwa na mambo yatakwenda vizuri,” amesema Msuva.

Habari kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 21, 2022
Kagere, Ndemla kuikosa Geita Gold