Mbunge wa Shinyanga Mjini, Steven Masele anatarajiwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Bunge kufuatia kutuhumiwa kuendeleza vitendo vya utovu wa nidhamu na kuwachonganisha viongozi wa Serikali na Bunge.

Mbunge huyo amewasili nchini mwishoni mwa juma lililopita akitokea nchini Afrika Kusini alipokuwa akilitumikia Bunge la Afrika (PAP), ambapo alikuwa kwenye mgogoro na Rais wake, Roger Dang ambaye alituhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka.

Akizungumza na vyombo vya habari mwishoni mwa juma lililopita, Spika Ndugai alimtaka kiongozi huyo kufika kuhojiwa kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge Jumatatu majira ya saa 5 asubuhi.

“Steven Masele hawezi kukaidi zaidi kwa sababu ni lazima arudi Tanzania, labda awe mkimbizi na akirudi lazima aje kwenye Kamati ya Maadili, tunachomuitia ni tabia yake ya uchonganishi wa viongozi, hatuwezi kusema ila mtaelewa fitina ikoje, ambayo ni kukosa sifa kwa kiongozi,”amesema Ndugai

Hata hivyo, Masele amebainisha kuwa ataweka kila kitu wazi mbele ya waandishi wa habari juu ya kilichotokea mpaka kumfikisha kwenye kikao cha nidhamu cha kamati ya maadili ya Bunge.

Video: Stonebwoy ahatarisha maisha ya Shatta Wale
Schwarzenegger amsamehe aliyempiga teke Afrika Kusini

Comments

comments