Bendera ya Tanzania inazidi kupepea kwenye kona ya burudani na michezo duniani, ambapo hivi karibuni mrembo Koku Gonza amefikisha jina la nchi yetu ndani ya Tamthilia maarufu zaidi kwa sasa nchini Marekani ya ‘Empire’.

Koku Gonza

Koku ambaye ni muigizaji na muimbaji aishie nchini Marekani ameonekana kwenye Tamthilia hiyo msimu mpya (msimu wa tatu) akimfundisha kucheza piano moja kati ya wahusika wakuu, rapa ‘Raheem’.

Mrembo huyo wa Tanzania ameshafanya kazi kadhaa ambapo mwaka 2011, wimbo wake wa Love ulikutoa album iitwayo Radiozophrenic. Moja kati nyimbo zinazounda album hiyo uitwao ‘L.O.V.E’ ulipata nafasi ya kuchezwa mara kadhaa kwenye vituo vikubwa vya BET, Channel O, MTV na vingine.

Anauwezo mkubwa wa kucheza piano, guitar na vyombo vingine vya muziki, huku muziki wake ukiakisi pia kabla lake la ‘Kihaya’.

Huu ni moja kati ya nyimbo zake:

CUF watoa msimamo wao rasmi na watakavyoishi na Serikali ya Dk. Shein
Misri Kujiuliza Tena Kwa Serengeti Boys Kesho