Polisi katika mji wa Samrala wameripoti kumkamata Mwanamke, Mtanzania anayejihusiha na mitindo  akiwa na gram 300 za Dawa za Kulevya aina ya Heroin.

Afisa wa Jeshi la Poisi, SSP- Khanna Navjot Singh Mahal amesema walipokua katika doria walimuona Mwanamke huyo akiwa amesimama huku ameshikilia begi dogo na mfuko wenye biskuti. Mwanamke huyo mara baada ya kuwaona Askari hao alianza kula Biskuti hizo, alipopekuliwa ndipo akabainika kuwa na Dawa hizo.

Afisa Jeshi la Polisi amezungumza na vyombo vya habari na kusema hii ni mara ya kwanza nchini kwao kumkamta mtanzania anayejihusisha na bishara ya dawa za kulevya.

Mwanamke huyo baada ya kuhojiwa alidai kuwa anatokea Jiji la Delhi na anafanya kazi za mitindo hata hivyo alikuwa akipeleka Dawa hizo kwa ajili ya kuwauzia watu kadhaa kwenye mji wa Ludhiana.

 

Ben Pol: Nimeshafanya kolabo na Chidima, sasa zamu ya Trey Songs
Afanyiwa upasuaji wa ubongo akiwa anapiga gitaa