Mwenyekiti Kamati ya muda ya uongozi wa CUF, Julius Mtatiro amejibu baadhi ya hoja za watu ambao wanataka CUF kukubaliana na Professa Lipumba kwa kuwa Mwenyekiti huyo ameshika makali kutokana na vyombo mbalimbali vya Serikali kumtambua.

Amesema kuwa hilo ni jambo ambalo halitawezekana tena kwao kukubali yaishe, hivyo hawawezi kukaa meza moja na Profesa Ibrahim Lipumba kwani alishaga jiuzuru katika harakati za Kampeni za uchaguzi.

“Ni mara kumi kumsamehe jirani yako aliyembaka mwanao, kuliko kumsamehe baba yako mzazi aliyembaka mwanao. Adui wa ndani, ni hatari zaidi kuliko adui wa nje. CCM ni adui bora kuliko Lipumba na kwa hiyo ni rahisi sana kufanya kazi na CCM kuliko kufanya kazi na Lipumba,”amesema Mtatiro

Aidha Mtatiro amesema kuwa ni rahisi sana kufanyakazi na Chama cha Mapinduzi CCM kuliko kufanya kazi na Profesa Ibrahim Lipumba kwakuwa alichokifanya si kitendo cha kiungwana.

Hata hivyo, Julius Mtatiro kwa sasa yupo nchini Marekani alipokwenda kimasomo na ayasema hayo kupitia mtandao wake wa Facebook na kusema ni jambo ambalo halitawezekana wao kukubali yaishe. 

 

Samia amuwakilisha JPM mkutano wa wakuu wa nchi SADC
Umoja wa mawakala wa pembejeo waomba kuteta na JPM