Hatimaye kikosi cha Mtibwa Sugar kimepata ushindi wake wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22, kwa kuifunga Kagera Sugar 1-0.

Mtibwa Sugar ikicheza nyumbani Mkoani Morogoro imejihakikishia ushindi huo wa kwanza msimu huu, kupitia kwa Riphat aliyepachika bao hilo pekee Dakika ya 13.

Mtibwa Sugar ilikua haijapata ushindi katika michezo saba iliyopita, hali ambayo iliifanya klabu hiyo Kongwe katika Ligi Kuu kuburuza mkia.

May be an image of 2 people, people playing sport, grass and text

Ushindi huo unaiwezesha Mtibwa Sugar kufikisha alama 5, ambazo zinaendelea kuwaweka mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba SC yaigomea GSM
Singo: Maandalizi Mchezo wa Miaka 60 ya Uhuru, Tanzania Vs Uganda