Mtoto wa Winnie Mandela, Zenani Mandela, amefunguka mbele ya umati mkubwa wa waombolezaji wakati wa mazishi ya mama yake yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Orlando, Afrika Kusini, ambapo amesema kuwa mama yake aliporwa haki yake wakati wa maisha yake.

Zenani alivicharukia vyombo vya habari na kusema kuwa vilitumika kumchafua mama yake, na vimepora urithi wa haki ya mama yake wakati wa uhai wake, huku akihoji kwa nini vyombo hivyo viliukalia ukweli na kusubiri mpaka mama yake afe, amehoji Zenani pindi akihutubia wakati wa salamu za mwisho za kumuaga mama yake..

Aidha, Zenani amesema wote waliomfanyia mabaya mama yake wasifikiri familia itayasau mabaya hayo.

Amedai kuwa ”Kumsifia sasa hivi, kumeonyesha wazi jinsi ulivyo unafiki” amesema Zenani.

Ameongezea kuwa Maumivu aliyoyapata mama yake yapo maishani mwake kwao pia.

Leo maelfu ya watu wamekusanyika katika uwanja huo kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho mbele ya mwanamapinduzi huyo wa Afrika Kusini, Winnie Mandela  ambaye pia aliwahi kuwa mke wa Nelson Mandela.

Baba wa mtoto mwenye asili ya China kutafutwa
10 Watiwa mbaroni kwa kuhamasisha maandamano

Comments

comments