Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu (Kazi, Ajira,bunge ,Uratibu, Vijana na wenye ulemavu) Jenista Mhagama amezionya taasisi za fedha zilizoanzishwa kwa lengo la kutapeli wastaafu kwa mikopo ya riba kubwa isiyo na tija wala maendeleo.

Ameyasema hayo leo Agosti 4, 2021 wakati akifungua na kufunga Semina kwa Wastaafu Watarajiwa iliyoandaliwa na Mfuko wa Uhifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma(PSSSF) Jijini Dar es Salaam yenye kauli mbiu “Elimu ya uwekezaji kwa Maisha endelevu baada ya Kustaafu”.

Aidha Waziri Mhagama amesema, kumekuwa na changamoto ambazo wastaafu wamekuwa wakikumbana nazo baada ya kustaafu na wakati mwingine kabla hata ya kustaafu ikiwa ni pamoja na kutapeliwa fedha zao.

“Niwaombe Wastaafu Watarajiwa kuweni na utaratibu maalumu wa kutoa taarifa ukiona wanaohisiwa ni matapeli ili tuweze kuwakamata na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.Kupitia hivyo tutaweza kuepukana na utapeli unaotokea mar kwa mara kwa wastaafu wetu,” Amesema Waziri Mhagama.

Amesema kuwa kupitia mafunzo hayo ni wakati mwafaka kumsaidia kuwaza kujipanga na kufanya maamuzi kuliko kumuacha akafanya maamuzi baada yya kustaafu, huku akisisitiza Serikali kuendelea kuunga mkono mafunzo hayo ili yaweze kuwa na tija kwa wastaafu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA. Hosea Kashimba amesema hadi kufikia mwezi Juni, 2021, mfuko ulikuwa na wanachama 705,484 ambao ni watumishi wa Umma na wafanyakazi wa makampuni ambayo Serikali inamiliki hisa zaidi ya 30%.

TFNC yaja na suluhu ulishaji wa watoto kwa njia ya mtandao (E- Learning)
Dkt. Mpango atoa pole familia ya Kwandikwa