Muigizaji Taraj P Henson maarufu kama Cookie ambaye ni staa wa tamthilia maarufu ya ‘Empire’ ameweka wazi kuwa amejiunga rasmi na timu kubwa ya mashabiki wa msanii wa Nigeria, Davido.

Taraj amepost kwenye instagram picha inayoonesha akisikiza wimbo wa Davido ‘How Long’ aliomshirikisha Tinashe, wimbo unaopatikana kwenye Extended Play ya mwimbaji huyo, ‘Son of Mercy’.

“Anybody who knows me know I LOVE MUSIC!!! Especially WORLD MUSIC!!! Thank you @tymwallacehair for turning me on to another heater!!!” ameandika kwenye picha hiyo.

Naye Davido aliiona hiyo kama fursa kwake na akawasilisha ombi lake rasmi kwa muigizaji huyo, kuomba nafasi ya kualikwa kwenye tamthilia hiyo kubwa.

“Big ups @tarajiphenson… LET ME BRING THAT AFRICAN HEAT TO EMPIRE!! ONE EPISODE IS COOL FOR ME LO,” Davido aliandika Instagram.

Empire huwaalika wasanii wakubwa kuwa wageni maalum, baadhi ya wasanii waliowahi kushiriki ni pamoja na Alicia Keys, Sonoop Dogg na wengine.

Sol Campbell Aipa Ubingwa Chelsea, Awafananisha Na Leicester City
Kauli ya Mashali kuhusu chanzo cha kupigwa kabla ya kufa yawekwa wazi, ”ni sh 1000!”