Klabu ya Young Africans kupitia kwa mwenyekiti wake Dr.Mshndo Msola imemtangaza kocha mzawa Juma Mwambusi kama kocha wa muda hadi mwishoni mwa msimu huu.

Msolla ametangaza maamuzi hayo, baada ya kumtimua kocha kutoka nchini Burundi Cedrick Kaze usiku wa kuamkia jana Jumatatu, kufautia matokeo ya kufungwa na Coastal Union ya Tanga 1-0, kabla ya kulazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania.

Juma Mwambusi anarudi kwenye benchi la ufundi la Young Africans ikiwa ni baada ya majuma kadhaa tangu aondoke kwenye nafasi ya kocha msaidizi kwenye klabu hiyo, kwa sababu za kiafya.

Mwambusi alijiweka kando ndani ya Young Africans baada ya michuano ya Kombe la Mapinduzi 2021 visiwani Zanzibar, ambapo klabu hiyo ilitawazwa kuwa mabingwa kwa kuifunga Simba SC kwa changamoto ya mikwaju ya Penati.

Kwa sasa Young Africans ipo nafasi ya kwanza na ina alama 50 kibindoni ndani ya Ligi Kuu Bara ambapo ilianza mzunguko wa kwanza ikiwa na Mwambusi pamoja na Kocha Mkuu, Zlatko Krmpotic ambaye naye alifutwa kazi.

Baadhi ya wachezaji wa Young Africans ambao hawajaitwa kwenye timu za taifa, wanatarajiwa kuingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya michezo ijayo ya Ligi Kuu pamoja na Kombe la Shirikisho.

Prince Dube aumia tena Azam FC
'Jembe Ulaya' awashauri viongozi Young Africans