Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Briar Cliff nchini Marekani amefariki dunia baada ya kuanguka kutoka kwenye ukingo wa mwamba alipokuwa anapiga picha ya pamoja na wenzake katika msitu wa Ozark-St. Francis.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Associated Press, Andrea Norton mwenye umri wa miaka 20 alifariki Jumamosi baada ya kuanguka umbali wa futi 100 kutoka kwenye ukingo huo wa mwamba.

Alianguka akijaribu kujipanga vizuri kwa kuweka nafasi ili rafiki zao pia waingie kwenye eneo la picha

Eneo hilo la ajali linafahamika pia kwa jina maarufu Hawksbill Crag na limewahi kutajwa kuwa kati ya maeneo muhimu yanayovutia kwenye makala maarufu ya ‘Top 10 Places to Kiss’, katika eneo hilo maharusi hukusanyika kwa ajili ya kupiga picha. Eneo hilo la msitu lina miamba na maporomoko ya maji.

Katika tovuti ya eneo hilo, kuna onyo lililotolewa kwa ajili ya kuwatahadharisha watu wanaokwenda kufurahia mandhari nzuri, “Tahadhari: Tafadhali kuwa makini na eneo hilo. Ni eneo zuri sana, lakini pia ni eneo hatari sana. Ni muhimu kuwa mwangalifu na kujihadhari usiende kwenye kingo za miamba, na weka uangalizi muhimu zaidi kwa watoto.”

Msemaji wa Chuo Kikuu cha Briar Cliff amekaririwa na mtandao wa Yahoo akithibitisha kutokea kwa kifo cha mwanafunzi huyo aliyekuwa kwenye harakati za kupiga picha na wenzake.

Mkate wageuka anasa Zimbabwe, bei yapaa
Beyonce alivyotikisa mitandao na ‘sapraiz’ ya albam, Makala

Comments

comments