Anthony Martial ameripotiwa kuwa hana mpango wa kuihama Manchester United na kwenda kujiunga na klabu ya matajiri wa jiji la ufaransa Paris Saint-Germain msimu ujao.

Nyota huyo kinda mwenye umri wa miaka 20, yupo kwenye kiwango kizuri hivi sasa tangu alipojiunga na United kwa da ya pauni milioni 36 akitokea klabu ya Monaco mwanzoni mwa msimu huu, baada ya kuitolea nje klabu ya iliyokua ikimuhitaji.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, ameshaifungia United magoli 12 katika mechi zote zikiwemo za kombe la FA na kiwango chake kinatajwa kuwa ni cha hali ya juu.

Alipoulizwa kama ni kweli ana mpango wa kuihama United  nakwenda kujiunga na PSG, Martial amesema  “United siyo timu iliyo bora kwa sasa lakini msimu ujao nina imani itafikia kiwango bora.

Manchester United inashikilia nafasi ya 6 kwa sasa katika msimamo wa ligi huku ikiwa inamiliki pointi 50,na Martial amefikisha idadi ya magoli 7 mpaka sasa katika nafasi ya 19 kwa wafungaji.

Dk. Shein aanza kupanga safu yake, Amteua Balozi Seif Ali kushika nafasi hii
Arsene Wenger Aendelea Kukingiwa Kifua Ili Asiondoke