Mshiriki wa Big Brother Africa (BBA) 2013 wa nchini Nigeria, Beverly Osu ameshambuliwa vikali mtandaoni mara baada ya kuonekana amelidhihaki vazi la masista la utawa kwa kulivaa na kupiga nalo picha huku akiwa ameshika na kuvuta sigara na kurusha mtandaoni picha hiyo.

Beverly Osu aliamua kuwajibu mashabiki hao kwa kusema kuwa yapo maovu mengi yanayofanywa na masista ikiwa pamoja na kuvuta sigara lakini pia yapo maovu yanayofanywa na mapadre ikiwa pamoja na kuwabaka masista, amehoji juu ya maovu hayo kukaliwa kimya ilihali yeye amepiga picha ya kisanaa na kushambuliwa vikali.

Kupitia ukurasa wake wa instagram amesema

”Nimezaliwa na nimekuwa nikifanya vitu vya Kikatoliki najua kuwa mnachukulia imani ipasavyo, watu inabidi wapate wasiwasi na kuombea waathirikia zaidi ya elfu moja ambao wanabakwa na kunyanyaswa na mapadri”

“Duniani kwa ujumla utakuta wahanga elfu moja wamebakwa na mapadri 300 Pennsylvania na sasa hivi watu wanaongea kuhusu picha ambayo ni sanaa, Iwapo mapadri na masista wanavuta sigara kwenye maisha ya uhalisia kitu ambacho hakijapingwa bado kama dhambi”

“Wapendwa Wanigeria sifanyi nachokifanya kwaajili ya kupata pongezi zenu, hii picha ingekuwa ya filamu ingekuwa sawa? inafurahisha pale mlipotenda dhambi kwaajili tu ya picha”

 

Kitendo hiko kimenukuliwa kuwa ni udhalilishaji na kwamba hajaitendea haki dini ya kikikristo pamoja na masista wa dini hiyo.

 

Video: Rais mwenye mshahara mdogo aliyejipunguzia nusu ya mshahara wake
TCRA yainyooshea kidole mitandao inayorusha maudhui bila usajili

Comments

comments