Mwandishi wa ngoma kali zilizowatoa waimbaji kutoka Mwanza, Barakah Da Prince na Mo Music na kuwafanya mashabiki kushangweka kila wanapozisikia, Lollipop amesema kuwa nyimbo hizo za Bongo Flava hazimpi amani hata kidogo.

Lollipop ambaye pia ni mtayarishaji wa muziki na muimbaji wa nyimbo za injili, ameandika na kuandaa ‘melodies’ za hits kama ‘Basi Nenda’ ya Mo Music, ‘Nivumilie’, ‘Siachani Nawe’ na nyingine za Baraka Da Prince na hivi karibuni aliandika hit ya ‘Moyo Mashine’ wa Ben Pol.

Lollipop kwenye cover ya albam yake ya Injili

Lollipop kwenye cover ya albam yake ya Injili

Lollipop aliiambia XXL ya Clouds Fm kuwa uandishi wa nyimbo hizo kali na uimbaji wa Bongo Flava sio kitu ambacho kinampa raha na amani hata kidogo kwani anaona kama zinamuweka mbali na Mungu wake.

“Siwi na amani kuimba Bongo Flava. Yako mengi yanayopelekea mimi nisiwe na amani, kwanza kabisa tangu nikiwa mtoto, moyo wangu umekuwa dedicated sana kwa Mungu. Kwahiyo mimi huwa naamini tu sijaumbwa kufanya hicho. Ninapojaribu kufanya moyo wangu haunipi go ahead,” alisema.

“Kuna kitu hata wewe unaweza kukifanya kwa moyo na unafurahi kukifanya na mimi ndivyo nilivyo, kwahiyo hata kazi ya production nafanya kwa moyo lakini sifurahii kama ambavyo nakuwa nafanya ngoma za gospel,” aliongeza.

Lollipop amekuwa akiandika nyimbo na kuzitengenezea melody tayari kwa wasanii kuzirudia tu na kuwa zao, na hivi sasa amekuwa akifanya kazi kwa karibu na watayarishaji wawili wa muziki, Kidbwoy wa Tetemesha Records na Nasda.

Video: Wabunge wavaa roho mbaya. Ni vita ya polisi, Zitto. Mkapa ajuta - Magazeti Juni 16 2016
Ongezeko la ubakwaji na ulawiti kwa watoto laongezeka