Naibu waziri wa elimu sayansi na teknolojia William Olenasha ameiomba serikali ya ufaransa kuwa na somo la Kiswahili katika mitaala yao ya kufundishia vyuo vya elimu ya juu nchini ufaransa.

Ole Nasha ametoa ombi hilo Jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa wanafunzi zaidi ya 900 katoka vyuo vikuu mbalimbali vya hapa nchini pamoja na wanafunzi wawakilishi wa vyuo vikuu kadhaa kutoka ufaransa waliokutana kujenga ushirikiano wa kusaidiana katika masuala ya elimu.

Mkutano huo umefanyika sambamba na kusaini makubaliano ya kusaidiana katika sekta ya afya kwa elimu na utafiti kati ya chuo kikuu kishiriki cha sayansi na tiba Muhimbili (MUHAS) na chuo kikuu cha afya cha Bordeaux kilichopo nchini ufaransa.

Aidha Ole Nasha amesema Serikali inakusudia kufanya mapinduzi katika sekta ya elimu kwa kuhakikisha elimu inayotolewa hapa nchini inamjenga mwanafunzi aweze kujiajili kadhalika awe na ubunifu kuajili wengine.

“Serikali ya ufaransa ina utaratibu wa kutoa ufadhili kwa wanafunzi 30 kusoma elimu ya juu nchini ufaransa kwa mwaka huu wameamua kufadhili wanafunzi 50, na leo wametukutanisha kuwapa elimu wanafunzi hawa wa elimu ya juu wapate uelewa wa masomo yanayofundishwa katika vyuo vya ufaransa ili waweze kuchagua ni wapi wanapenda kupata elimu itakayojibu ndoto zao” Amefafanua Naibu waziri

Kwa upande wake balozi wa ufaransa nchini Frederick Clavier amesema leo wamekutana kuandaa dira mpya ya mashirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na ufaransa katika sekta ya elimu ili kuhakikisha wanafunzi wanahimili ushindani katika soko la ajira la kimataifa.

“Kuna wahitimu wengi hawana ujuzi wa kujua ni kwa namna gani ajiajiri au atengeneze ajira badala yake wanategemea kuajiliwa. Sasa kwa namna tunavyozungumza tunataka wahitimu wote wa elimu ya juu wawe na uwezo mkubwa wa kupambanua mambo kulingana na nyakati na mazingra, hii itapunguza umaskini nchini Tanzania.” Amesema Balozi.

Naye mmoja wa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kutoka chuo kikuu cha kilimo Sokonine Ahmed Abdul amesema amefurahishwa na yaliyojili katika mkutano huku agenda yake ya kuwafundisha marafiki zake na wajuani wake waondoe fikra hasi za kungoja ajira vijiweni na badala yake wajikite katika kujiajiri.

Video: Hoja 4 kumng'oa Mbowe Chadema, Watoto watatu wa familia moja wafa maji baharini Dar
TFF yatoa tamko kwenye dirisha la usajili