Msanii wa bongo fleva Faustine Charles Mfinanga maarufu Nandy ametangaza balaa litafanyika leo, Jumamosi, Septemba 4, 2021 katika Viwanja vya Posta jijini Dar ambapo kutakuwa na lile tamasha lake kubwa la Nandy Festival 2021.

Nandy amesema kuwa, kila kitu kipo sawia kabisa kwa ajili ya burudani ambayo ameahidi itakuwa ya kihistoria

“Naomba nisiseme sana, lakini kama nilivyosema, Dar ndiyo kilele kikuu na Dar ndipo tunapoishi asilimia kubwa ya wasanii kwa hiyo itakuwa balaa juu ya balaa”.amesema Nandy

”Mashabiki wafurike kwa wingi kwa sababu itakuwa hatari, kwa sasa tupo Jumba la Nandy Festival, maandalizi yote yamekamilika, kinachosubiriwa ni muda tu watu wakale burudani kama yote,”amesema Nandy

Waziri Mkuu aagiza bei mpya za mafuta ziangaliwe upya
Bilioni 212.95 kununua ndege 5