Waziri wa habari,Utamaduni,Sanaa na michezo Nape Moses Nnauye amezidi kusisistiza na kuwaonya wale wote wanaoanza kuhujumu mfumo wa matumizi ya tiketi za Elekroniki ambao unaanza kutumika rasmi kuanzia Jumamosii hii katika mechi ya watani wa Jadi klabu ya soka ya Simba na Yanga.

Akizungumza na waandishi wa habari Nape amesema kumekuwa na watu wanoanza kuhujumu mfumo huo wa tiketi za Elekroniki ambao wanasababisha kuonekana kama haujakamilika katika uanzaji wake.

Kwa upande mwingine nape ameelezea jinsi mkataba wa tiketi za Elecktoniki ulivyosainiwa na kuelekezea kuwa tiketi hizo kwa sasa zinatolewa bure pasipo malipo yoyote yale.

Ligi Kuu Ya ZFA Msimu Wa 2016/17 Ipo Mbioni Kuanza
Serikali yakanusha tangazo la ajira lililosambazwa