Msanii wa Hip Hop nchini, Nash Mc kesho Machi 19, 2017 anaachia wimbo wake mpya unachokwenda kwa jina la Shujaa. “Nawakumbusha kuwa kile ambacho mlikua mnakikosa mashabiki, wakereketwa na wapenzi wa Hip Hop ndio hicho kinachokuja kwenye Shujaa” amesema Nash Mc.

Nash Mc amesema kuwa Shujaa ni wimbo unaokuja rasmi kuutambulisha ujio wake mpya ambapo amewataka watu wote ambao wanafuatilia kwa ukaribu ujio wake huo kuwa tayari kupokea kitu kizuri na cha tofauti.

“Nimeanza kutumiwa ujumbe na makamanda wengi sana wakiulizia jinsi ya kupata wimbo huo, Ukweli ni kwamba Kibao hiko kitatoka rasmi siku ya Jumapili 19/03/2017”.

Pia Nash Mc ameweka wazi namna ya kuupata wimbo huo ambapo ameeleza kuwa njia ya kwanza itakayotumika kusambaza wimbo huo ni kwa WhatsApp tu kisha baada ya hapo utawekwa sehemu ambazo mashabiki na wapenzi watapakua wimbo huo. Nash Mc amesema wimbo huo hautauzwa mahala kokote.

Aidha, Nash Mc amesisitiza na kuwataka mashabiki wake kutambua kuwa yeye hatabadilika daima atadumu kwenye utamaduni wa Hip Hop kwa hali yoyote.
“Nikifa maskini wewe furahia”.

Lowassa atoa ya moyoni kuhusu zuio la wabunge wa CCM
Video: Ukweli kuhusu radi za kichwani Sumbawanga, Ridhiwani afunguka baada ya kuhojiwa