Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema kuwa njia bora ya kukabiliana na changamoto ya ukusanyaji wa Takwimu za kiutendaji wa kila siku katika wizara, Idara na taasisi za umma ni kuwa na mfumo wa uratibu wa takwimu hizo chini ya kituo kimoja cha uratibu.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dkt. Albina Chuwa alipokuwa akizungumza na Waganga wa mikoa na Waganga Wafawidhi.

“Lengo letu ni kuwa na kituo kimoja cha takwimu za afya ambacho takwimu zote za afya zinapatikana hapo kuanzia vifo na uzazi, idadi ya madaktari na watumishi wa afya, elimu yao, uzoefu wao na hata madawa yalipo hospitalini na iwe ni rahisi mtu kuzipata,” amesema Dkt. Chuwa

Aidha, amefafanua kuwa kufanya hivyo kutawezesha kufanya uchambuzi wa kina wa viashiria mbalimbali kwa kulinganisha viashiria husika na upatikanaji, utayari, ubora matumizi ya huduma zitolewazo.

Hata hivyo, Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa kati ya vyanzo vingi vya takwimu za afya kimojwapo ni takwimu za kiutawala ambazo kama ilivyo katika sekta nyingine ukusanyaji wake unahitaji maboresho makubwa.

 

Bei ya mifugo yapaa sokoni
Man Utd yalinda kibarua cha Mourinho, yaweka kando ya Zidane