Kaimu kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Ettiene Ndayiragije, ametaja kikosi cha wachezaji 25, kitakachoingia kambini leo jumatatu, tayari kwa maandalizi ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa kuwania kufuzu fainali za mataifa bingwa Afrika (CHAN) dhidi ya Sudan.

Stars itaanzia nyumbani Dar es salaam mwishoni mwa juma hili, kisha itakwenda kumalizia mchezo wa mkondo wa pili mjini Khartoum mwezi ujao, na kama itafanikiwa kushinda itajikatia tiketi ya kushiriki fainali za CHAN zitakzounguruma nchini Cameroon mwakani.

Kikosi kilichotajwa na kocha Ndayiragije kwa ajili ya mchezo dhidi ya Sudan.

Magufuli ampongeza Mtaturu kutwaa jimbo la Lissu
Kipa bora azawadiwa bunduki aina ya AK-47