Ndege aina ya Boeing 737 MAX 8  ya shirika la Lion Air  imeanguka baada ya  kupaa kutoka uwanja wa ndege mjini Jakarta

Maafisa wa Indonesia wamesema ndege hiyo  yenye nambari JT-610 ilikuwa safarini kutoka mji mkuu wa Indonesia kwenda Pangkal Pinang, jiji linalopatikana katika visiwa vya Bangka Belitung iIitoweka kutoka kwenye mitambo ya rada saa kadha baada ya kupaa, ilipokuwa inavuka bahari

Hata hivyo haijabainika mara moja ni abiria wangapi walikuwa ndani ya ndege hiyo wala chanzo cha ajali hiyo kuanguka bado hakijajulikana.

Msemaji wa shirika la huduma za uokoaji na kuwatafuta manusura, Yusuf Latif amewaambia wanahabari kuwa Imethibitishwa kwamba ndege hiyo imeanguka.

Aidha Afisa mkuu mtendaji, Edward Sirait ameambia shirika la habari la Reuters: “Hatuwezi kusema chochote kwa sasa. Tunajaribu kutafuta maelezo na data zaidi.”

Tanjung Priok  afisa wa bandarini amenukuliwa na vyombo vya habari  Indonesia  akisema kwamba maafisa wa boti wa kusindikiza meli wameripoti kwamba wameviona vifusi vya ndege hiyo kwenye maji.

Ndege hiyo safari namba JT-610 iliondoka Jakarta saa 06:20 saa za huko Jumatatu asubuhi (23:30 GMT Jumapili).

Mtaalamu wa masuala ya uchukuzi wa ndege Gerry Soejatman ameambia BBC kwamba ndege hiyo aina ya MAX 8 imekuwa ikikumbwa na hitilafu tangu ilipoanza kutumiwa.

Waziri aomba radhi kuvuja kwa picha zake za ngono
TCRA yamfungulia kesi Wema