Mshambuliaji kutoka nchini Sweden Zlatan Ibrahimovic amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuitumikia Manchester United.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35, alifunga mabao 28 katika michezo 46 aliyocheza na Man Utd kwa mara ya kwanza msimu uliopita, akitokea kwa matajiri wa jijini Paris nchini Ufaransa PSG.

Zlatan atavaa jezi namba 10 msimu huu, na anatarajiwa kurejea uwanjani kwa mara ya kwanza Oktoba 28 katika mchezo wa ligi ya England dhidi ya Tottenham.

Kwa mara ya mwisho Zlatan alionekana akiwa na jezi za Man Utd mwezi April wakati wa mchezo wa Europa League dhidi ya Anderlecht ya Ubelgiji, kabla ya kupata majeraha ya misuli ya paja, ambayo yalimuweka nje hadi mkataba wake wa mwaka mmoja ulipofikia kikomo Juni 30 mwaka huu.

Maya Yoshida Anogewa St Mary's Stadium
Video: LHRC wasema mahakama imepuuzwa, walaani kukamatwa Tundu Lissu