Mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi (NEC), Ramadhani Kailima amesema tume ya uchaguzi imejipanga kuanza kutoa elimu katika kipindi hiki cha chaguzi wa marudio, elimu ambayo itakuwa ikigusia mada mbalimbali za uchaguzi ikiwemo haki na wajibu wa mpiga kura.

Kailima amesema hayo alipokaa kikao na watendaji wa tume ya uchaguzi mdogo unatarajiwa kufanyika jumamosi ijayo ambayo itakuwa Februari 17, 2018.

Hata hivyo zikiwa zimebaki siku tano kufanyika kwa uchaguzi huo wa marudio katika jimbo la Kinondoni na Siha pamoja na kata nne.

Tume ya Uchaguzi ya Taifa NEC, imedai maandalizi yanaendelea vizuri ikiwa pamoja na kutatua changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza.

Huu ndio ukweli kuhusu ndoa ya AY
Video: Lowassa akoleza moto waraka wa Maaskofu, Mkuu usalama CDM aanika mbinu sita

Comments

comments