Aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Marouane Chamakh amekamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Cardiff City inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini England.

Chamakh, amejiunga na Reading baada ya kuachwa huru na  klabu ya Crystal Palace mwishoni mwa msimu uliopita, hivyo kanuni za usajili zimemruhusu kusajiliwa katika kipindi hiki ambacho tayari dirisha limeshafungwa tangu mwishoni mwa mwezi Agosti.

Kanuni za usajili wa wachezaji nchini England zinatoa nafasi kwa klabu kufanya usajili wa wachezaji walio huru katika kipindi hiki, pasi na kuzingatia dirisha kufungwa.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32 kutoka nchini Morocco anakua mchezaji  watatu kusajili wa meneja wa Bluebirds Neil Warnock ambaye amedhamiria kuirejesha Cardiff City ligi kuu ya England msimu wa 2017/18.

Wachezaji waliomtangulia Chamakh klabuni hapo baada ya kusajiliwa na meneja huyo kutoka nchini England ni Sol Bamba pamoja na Junior Hoilett.

Samia Suluhu azindua mradi wenye thamani ya shil. bil. 4.5
Video: Waziri Mkuu apokea michango ya sh. mil. 660, tetemeko Kagera