Rapa kutoka Marekani Cornell Iral Haynes Jr maarufu kama Nelly amekamatwa baada ya mwanamke mmoja kudai rapa huyo alitaka kumbaka wakati wakiwa kwenye basi la ziara (tour bus) kuelekea kwenye tamasha la msanii huyo.

Hata hivyo Nelly amekanusha madai hayo na sasa ameachiwa huru wakati polisi wakiendelea na uchunguzi zaidi ili kubaini ukweli wa tukio hilo.

“Sina  hatia kabisa ni wazi tuhuma zilizotolewa juu yangu ni uongo, nina hakika kwamba ukweli utaonekana”, alisema rapa huyo.

Rapa huyo mwenye umri wa miaka 42 yuko katika ziara yake ya kufanya matamasha akiwa na kundi la Backstreet Boys na Florida Georgia Line na siku ya ijumaa alipiga showa huko Auburn.

Nelly aliyetamba na nyimbo kali kama ‘Dilema’ na ‘Hot in here’ alishawahi kukamatwa na polisi mwaka 2015 kwa kukutwa na bunduki na madawa kwenye basi lake la ziara.

Mji mkuu wa Ghana wakumbwa na mlipuko mkubwa wa gesi
Lema: Hakuna jipya baraza la mawaziri