Mshambuliaji wa klabu ya Paris Saint-Germain, Neymar ameitaka klabu yake mpya kumuuza mshambuliaji mwenzake Edinson Cavani baada ya wawili hao kuzozana kuhusu kupiga mkwaju wa penati.

Kulingana na taarifa za gazeti la ‘Spanish Outlet Sport’, Neymar ambaye ni mchezaji ghali zaidi duniani amemtaka mwenyekiti wa klabu hiyo Nasser Al-Khalifi kumuuza Cavani akisema kuwa uhusiano wake na Mshambuliaji huyo umeharibika na hivyobasi hawawezi kucheza pamoja.

Neymar Jr na Edinson Cavani waligombea kupiga penati iliyopatikana katikati ya mchezo ambao PSG iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya klabu ya Lyon.

Baada ya mchezo huo kuisha Cavanni alimfuata Neymar vyumbani na kumsema, Neymar alikasirika wakataka kupigana baada majibizano makali lakini nahodha wa klabu hiyo Thiago Silva alisimama kati yao na kusulushisha ugomvi huo.

Inaaminika kwamba Neymar anataka mshambuliaji huyo kuuzwa wakati wa kufunguliwa kwa dirisha la uhamisho mwezi Januari.

Inawezekana ugomvi wa Neymar na Cavani ni ubinafsi au pesa kwani inafahamika kwamba wachezaji hao wote wameahidiwa bonasi ambazo watapata kama wakimaliza kama wafungaji bora wa ligi, alichoahidiwa Neymar hakijafahamika lakini Cavanni ameahidiwa €1m kama akimaliza kileleni mwa ufungaji.

 

 

Picha: JWTZ waanza rasmi ujenzi wa ukuta kudhibiti madini ya Tanzanite
Agizo la Serikali juu ya matibabu ya Lissu