Klabu ya Paris Saint-Germain imeingiwa na wasiwasi mkubwa wa kumkosa mshambuliaji wake ghali zaidi duniani, Neymar kwa ajili ya mechi ya marudiano ya mashindao ya Klabu Bingwa barani Ulaya.

Hofu hiyo imekuja baada ya mshambuliaji huyo wa Timu ya Taifa ya Brazil kuumia kifundo cha mguu kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1 wakati PSG walipokuwa wakikabiliana na Marseille.

Mchezo wa marudiano baina ya PSG na Real Madrid unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Parc des Princes nchini Ufaransa siku ya Jumanne ya Machi 6 huku PSG ikihitaji ushindi wa bao 2-0 ili kufuzu kwa hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Klabu ya PSG ndiyo iliyotoa taarifa ya undani zaidi ya kuumia kwa mchezaji huyo huku vipimo zaidi vikiendelea kufanya kubaini muda utakaohitajika kwa mchezaji huyo kukaa benchi ili kupona majeraha aliyoyapata.

Hata hivyo Kocha wa Timu ya Real Madrid, Zinedine Zidane amemuombea dua mchezaji huyo aweze kupona kwa wakati ili awemo kwenye kikosi cha PSG kitakachokutana na Madrid.

“Sina furaha kwa kuumia Neymar, na ninatarajia atakuwemo kwenye kikosi tutakachopambana nacho. Nisingependa mchezaji wa wapinzani wetu awepo kwa sababu ya majeraha” amekaririwa Zidane.

PSG inatafuta nafasi ya kuingia fainali ya Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza kwenye historia yake.

Kilio cha Young Africans chasikika
Ramaphosa atangaza baraza jipya la Mawaziri