Ngome ya Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe imeendelea kupata mtikisiko ndani ya Jimbo la Hai mara baada ya Diwani wa Kata ya Romu, Shilimiafoo Kimaro kujiuzulu kiti chake na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Kimaro anakuwa diwani wa sita kupitia Chadema kuchukua uamuzi wa kung’atuka katika kiti chake na kujiunga na CCM.

Madiwani wengine waliomtangulia Kimaro katika mfululizo wa maamuzi kama hayo ni Yohana Laiza( Kata ya Kia), Everest Kimathi(Kata ya Mnadani), Abdalla Chiliwi (Kata ya Weruweru), Goodluck  Kimaro (Kata ya Machame Magharibi) na Robsoni Kimaro( Kata ya Uroki).

Aidha, Ikumbukwe kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 , Chadema kilipata madiwani katika Kata zote 17 za Jimbo la Hai.

Diwani wa hivi karibuni kabisa kujiuzulu kabla ya Kimaro ni Yohana Laiza ambaye alichukua uamuzi huo kwa sababu ya kile alichokisema kuwa anaunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na Rais Dkt. John Magufuli.

Laiza ambaye alitangaza uamuzi wake huo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Sanya Station na kuhudhuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya , alisema amechukua uamuzi huo kutokana na kuridhishwa na uamuzi wa mkuu  huyo wa Wilaya ambaye ni mpya,  kutembelea kata hiyo na kusikiliza kero za wananchi hususani mgogoro uliopo kati ya wananchi na uongozi wa Kiwanja cha Ndege cha KIA

 

Habari Picha: Spika Job Ndugai amjulia hali Dkt. Kigwangallah
Kikosi cha Brazil chatajwa, Marcelo, Miranda, Paulinho, Fernandinho, Jesus OUT