Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umemkabidhi mkuu wa Mkoa Kagera msaada wa Bati 50 ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali mkoani humo katika kuendelea kuboresha vituo na maeneo mbalimbali ya kutolea huduma ya Afya.

Zoezi hilo la kukabidhiana mabati hayo limefanyika katika viwanja vya ofisi za mkuu wa Mkoa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu tawala wa mkoa huo pamoja na wakuu wa wilaya.

Akizungumza mara baada ya kutoa msaada huo Kaimu meneja wa NHIF Mkoa Kagera, Dkt. Allen Kanjanja amesema kuwa wamekuwa wakifutilia kwa karibu harakati za ofisi ya mkuu wa mkoa katika kuhakikisha jamii ya mkoa huo inapata huduma iliyo bora ya Afya.

Amesema kuwa mfuko huo wa Taifa wa Bima ya Afya ni mfuko ambao unampango wa kumfikia kila mwananchi na sasa tayari wameanza katika vyama vya ushirika kwa kuwaunganisha wananchama wa vyama hivyo, na kuongeza kuwa watoa huduma katika vituo vya afya mbalimbali wanatakiwa kuwahudumia wanachama wa NHIF.

“Nitoe wito kwa watoa huduma, wanachama wanaponung’unika katika suala la kupata huduma ya Afya wakati tayari kailipia linakuwa sio jambo la kiungwana, tukumbuke hawa wananchama ndio wanaouendesha mfuko huu hivyo wahudumiwe kwa kiwango kinachofaa.” amesema Kanjanja.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali, Marco Gaguti amesema kuwa NHIF wamekuwa wakiijali jamii kwa kutoa misaada mbalimbali kwa jamii na kuwashukuru kwa msaada wa bati ambapo ameahidi kuwa msada huo utatumika kwa makusudi yaliyokusudiwa.

“Walikuja ofisini kwangu baada ya kuona nikitoa baadhi ya vitu kule wilayani Kyerwa na leo wamekuja kunikabidhi bati 50, kwa niaba ya uongozi wa mkoa na wanachi wa mkoa Kagera napokea bati hizi na ninaahidi kuwa zitatumika kwa makusudi yaliyokusudiwa katika kuimarisha huduma za Afya katika maeneo korofi ndani ya mkoa Kagera.” amesema Gaguti.

Mchezaji wa Algeria atimuliwa Timu ya Taifa kwa kuonesha makalio
Iran yapuuza wito wa Marekani, yaongeza uzalishaji wa madini ya Uranium

Comments

comments