Kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike yenye makao yake makuu nchini Marekani, imempongeza balozi wake Cristiano Ronaldo, kwa mafanikio aliyoyapata msimu wa 2016/17 kwa kumtengenezea viatu vipya aina ya Mercurial Campeões.

Viatu hivyo vya kisasa vimenakshiwa kwa rangi nyekundu ambayo ni rangi ya jezi ya timu ya taifa ya Ureno.Pia vina nembo ya kibiashara ya Ronaldo ya CR7, na kwenye visigino kuna nembo ya timu ya taifa ya Ureno.

Image result for Mercurial Campeões - cr7Image result for Mercurial Campeões - cr7

Ronaldo ataanza kuvaa viatu hivyo wakati wa fainali za kombe la mabara zitakazifanyika nchini urusi kuanzia mwishoni mwa juma hili.

Kwa mara ya kwanza Ureno itashiriki michuano ya mabara baada ya kuwa mabingwa wa Ulaya kupitia fainali za Euro 2016 zilizofanyika Ufaransa. Ureno waliwafunga wenyeji bao moja kwa sifuri katika mchezo wa fainali uliochezwa jijini Paris.

Irene Uwoya afunguka kuhusu ombi la Dogo Janja kummiliki
Jeshi la Polisi latoa tahadhali kwa wananchi, latoa onyo kali