Serikali kupitia ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI  imekabidhi vya darasa la nne katika Mkoa wa Njombe katika wilaya nne lengo likiwa ni kusaidia kuinua kiwango cha elimu katika shule mbalimbali za mkoani humo.

Takribani vitabu 30,355 vimekabidhiwa, mgawanyo wa vitabu hivyo ni kwamba Maarifa ya Jamii, 6906, Uraia 6906, Kiswahili 6858, Hisabati 5772, Kingereza 3913 huku Halmashauri ya Njombe ikiwa imepokea vitabu 4634.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Njombe, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri, Mwakilishi kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu TAMISEMI, Salum Mkuya wamesema utolewaji wa vitabu hivyo na serikali ni mkakati wa utekelezaji wa  ilani  ya chama cha mapinduzi CCM kuinua kiwango cha ufaulu mashuleni.

“Hatuna budi kumpongeza Rais wetu kwa kutekeleza ilani yetu, tumuunge mkono kwa uchapakazi wake mzuri na kuimalisha elimu katika nchi hii, kwa mkoa wa Njombe vitabu ambavyo vimesambazwa ni 30,355,” amesema Mkuya.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa, Ruth Msafiri aliwataka Walimu mkoani Njombe kuhakikisha vitabu vinatunzwa na vitumike kwa ajili ya kuinua elimu mkoani humo.

“Vitabu hivi vitachochea ufaulu katika mkoa wa Njombe, hususani kwenye Halmashauri ya Mji wa Njombe, ambapo mara zote haijashuka namba mbili kimkoa na inachuana na Halmashauri ya Makambako,” amesema Ruth.

Wanafunzi wa shule ya msingi Ruhuji, muakilishi wa katibu mkuu TAMISEMI na viongozi wa mkoa wa Njombe na wilaya wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa vitabu vya darasa la nne.

 

Malcom azikacha Everton, Tottenham atua Stadio Olimpico
Chancel Mbemba kucheza Ureno 2018/19

Comments

comments