Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu amesema kuwa anakusudia kuwasilisha muswada wa binafsi utakao weka sharti la kurejesha mjadala wa katiba mpya katika kikao cha tisa cha bunge kinachotarajiwa kuanza Novemba 7, 2017.

Ameyasema hayo hii leo kupitia mitandao yake ya kijamii ambapo amesema kuwa amekusudia kufikisha jambo hilo mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Job Ndugai.

“Nakusudia kuwasilisha kwa spika wa Bunge, Job Ndugai. azma yangu ya kuleta muswada binafsi wa sheria katika kikao kijacho cha Bunge itakayoweka sharti la kurejea upya mjadala wa Katiba Mpya ya Tanzania, kwa kuzingatia rasimu ya Katiba kama ilivyowasilishwa na Tume ya Jaji Warioba,”amesema Nyalandu

Hata hivyo, suala la Katiba Mpya licha ya kuwa siyo kipaumbele cha Rais John Pombe Magufuli lakini wadau mbalimbali wamekuwa wakilizungumzia wakisema kuna haja kubwa ya mchakato huo wa Katiba mpya kuendelea sasa wakidai kuwa huu ni wakati sahihi zaidi mchakato wa Katiba Mpya kuendelea.

LIVE BREAKING: Rais Magufuli apokea ripoti mazungumzo ya Serikali na Barrick
Waziri Kigwangalla kukutana na wadau wa maliasili na utalii