Kufuatia kubadilishiwa adhabu kwa msanii wa bongo movie nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, mama wa Marehemu Kanumba, Flora Mtegoa ameonekana kutoridhishwa na mabadiliko yaliyofanywa na Serikali juu ya kifungo cha Lulu.

Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili kwa kosa la kumuua Kanumba bila kukusudia aliingia gerezani Novemba 13, 2017 na kuachiwa huru kwa msamaha wa Rais mnamo Mei 12, Mei 2018 na miezi iliyobaki kukamilisha miaka miwili atatumikia kifungo cha nje kwa kutoa huduma kwa jamii ikiwa pamoja na kufanya usafi katika baadhi ya maeneo nchini.

Kiongozi wa wasanii wa bongo Movie, Steve Nyerere amesema amekasirishwa sana na Mama Kanumba kutoridhia msamaha aliopewa Lulu na kumshauri kuwa hawezi kushindana na maamuzi ya Serikali amedai kuwa alitakiwa kunyamaza na maisha yaendelee.

Nyerere amevuka mbali zaidi na kusema ameamua kufuta namba ya Mama Kanumba akidai kuwa hana shughuli naye tena amefanya hivyo mara baada ya kuona anaongea vitu ambavyo havina tija.
Steve amehoji kuwa hata kama Lulu angefungwa miaka 100 je Kanumba angerudi?, Ameongezea kuwa ”Usilazimishe watu au jamii yako ikuone umeshindwa, wala usiilazimishe jamii ikuone una roho mbaya, hapaswi kulalamika sana kwa sababu hana uhakika kama kweli aliua, lakini pia wawili hao walikuwa kwenye mahusiano,” amesema Steve.
Mstaafu 1, ajira 1, wahitimu 100,000 Nini kifanyike?
Video: Makonda awapa onyo kali wasichana wa mkoa wake

Comments

comments