Beki wa kati wa vinara wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Wekundu Wa Msimbazi Simba Juuko Murushid, ni miongoni mwa wachezaji 23 wa mwisho waliotajwa na kocha Milutin “Micho” Sredojovic kwa ajili ya kuunda kikosi cha Uganda (The Cranes) tayari kwa michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON 2017) itakayoanza hivi karibuni huko nchini Gabon.

Juuko ametajwa katika kikosi hicho baada ya kuonyesha kandanda safi katika kipindi chote cha michezo ya kuwania tiketi ya kufuzu kwa michuano hiyo.

Wakati Juuko akitajwa kikosini nyota wa zamani wa Simba SC Emanuel Okwi na Hamis Kiiza Diego wao hawakupata japo bahati ya kutinga kwenye kikosi cha awali cha wachezaji 27.

Aidha Micho ambaye aliwahi kukinoa kikosi cha Young Africans amewachagua wachezaji wanne pekee wanaocheza ndani ya Uganda.

Wachezaji hao ni Geoffrey Sserunkuma, Joseph Ochaya na Awany Shaban (Onduparaka).

Uganda imepangwa katika kundi D na itaanza michuano ya AFCON kwa kuvaana na Ghana Januari 17, na ya siku nne baadae wataivaa Misri katika dimba la Stade de Port Gentil.Uganda itafunga dimba kwa kucheza na Mali Januari 25 huko Stade d’Oyem.

Kikosi Kamili.

Makipa:Denis Onyango,Robert Odongkara na Salim Omar Magoola

Mabeki:Joseph Ochaya, Murushid Juuko,Isaac Isinde, Denis Iguma, NicholasWakiroWadada, Shafik Batambuze naTimothy Dennis Awany

Viungo: Tonny Mawejje,Khalid Aucho,Godfrey Walusimbi, Michael Azira, Hassan Mawanda Wasswa na Geoffrey Kizito.

Washambuliaji:Junior Yunus Sentamu, Geoffrey Sserunkuma, William Luwagga Kizito, Geoffrey Massa, Moses Oloya, Farouk Miya na Muhammad Shaban.

Mbora Wa Wabora Afrika Kujulikana Leo
Mchezaji Wa Ligi Daraja La Saba Kusajiliwa Arsenal