Kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Odinga aliyeshindwa katika uchaguzi wa urais uliopita amesema kuwa atafichua ushahidi wote uliotumika kuiba kura katika uchaguzi huo.

Odinga ambaye alikuwa anawania nafasi ya urais kwa mara ya nne mfululizo amesema kuwa hatowania tena nafasi hiyo hivyo amewataka Wakenya kujua kile kilichofanyika katika uchaguzi huo kilichopelekea kushindwa na mpinzani wake kutoka Jubilee, Uhuru Kenyatta.

Amesema ni lazima dunia ijue kile ambacho kimetendeka Kenya katika uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkubwa huku bado akishikilia msimamo wake kuwa katika uchaguzi alimshinda mpinzani wake, Uhuru Kenyatta.

“Leo tunataka kuionyesha dunia vile tulivyoibiwa na hawa Jubilee, ushahidi wote tunao, wizi kama huu haukubariki, hivyo naiomba tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC initangaze kuwa rais wa nchi ya Kenya,”amesema Odinga

Aidha, Odinga ameongeza kuwa hili sio suala la kuwa mbishi yeye kwakuwa anajua kabisa kwamba hatawania tena nafasi ya urais, hivyo lengo lake ni kutaka Wakenya waelewe kile kilichofanyika pamoja na ulimwengu mzima.

Hata hivyo, mwanasiasa huyo anadai kuwa Kompyuta za tume ya Uchaguzi ziliingiliwa na wadukuzi kuweka matiokeo yao yaliyompatia ushindi Uhuru Kenyatta ambapo anasema hakustahili.

LIVE: Rais wa Misri ahitimisha ziara yake Tanzania
Video: Ruby afunguka nje ndani kuhusu mpenzi wake mpya, ujio wake mpya