Pacha mmoja aliyebaki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ‘Rehema’ kati ya mapacha wawili waliotenganishwa Julai Mosi mwaka huu, amefariki dunia jana saa 5 asubuhi Agosti 11 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali hiyo.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano kwa umma, Muhimbili, Aminiel Aligaesha amethibitisha kutokea kwa kifo hicho akizungumza na Gazeti la Mwananchi.

“Ni kweli Rehema alifariki jana, Rehema amefariki dunia siku 32 baadaye tangu kifo cha pacha wake.” Alisema Aligaeshi.

Pacha Mwenzake ‘Neema’ alifariki Julai 10 mwaka huu ambapo hali yake ilibadilika ghafla akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) na alifariki dunia wakati akiendelea na matibabu Jumapili saa 3 asubuhi na alizikwa Julai 14 katika makaburi ya Ulongoni B yaliyopo Gongo la Mboto.

Watoto hao mapacha wawili wenye umri wa miezi tisa walizaliwa wakiwa wameungana sehemu ya kifua na tumbo na kwa upande wa umbo la ndani walikuwa wameungana ini ila kila Mtoto ana ini lake.

Tanzania ilikuwa nchi ya tatu Barani Afrika kufanya upasuaji wa aina hii baada ya Afrika ya Kusini na Misri.

Kenya: Wanahabari kujadili utoaji matokeo kwa kutofautiana
Kenya: Wakenya roho juu wakingojea matokeo ya uchaguzi mkuu