Meneja wa Arsenal Arsene Wenger, ameahidiwa kazi ya kukinoa kikosi cha mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain kwa mkataba wa miaka miwili.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na SunSport, umebaini kuwa, meneja huyo kutoka Ufaransa amekua chaguo la kwanza la PSG katika mipango ya kurithi mikoba ya Unai Emery, ambaye ameonyesha kushindwa kwenda sambamba na kasi ya mabingwa hao wa Ligue 1.

Mwenyekiti wa PSG Nasser Al-Khelaifi, amekua mstari wa mbele kumpendekeza Wenger kwenye harakati za kupewa benchi la ufundi la klabu hiyo, kutokana na falsafa za ufundishaji wake kuaminika huenda zikaivusha klabu hiyo na kufikia malengo ya kufanya vyema ndani na nje ya Ufaransa.

SunSport, mapema hii leo wameandika bado Wenger amekua na hali ya kujifikiria mara mbili kuhusu ofa hiyo, kwa kuamini huenda akawa na nafasi nyingine ya kusaini mkataba mpya ya kukinoa kikosi cha Arsenal.

SunSport wamedai kuwa, mapema mwezi huu, Wenger alikutana na viongozi wa juu wa Arsenal kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kuangalia uwezekano wa kusaini mkataba mpya, lakini pamekua hapana majibu ya kuridhisha, japo mzee huyo anatarajiwa kutangaza mustakabli wake siku kadhaa zijazo.

Wenger mwenye umri wa miaka 67, amepanga kuendelea kuwa meneja wa soka kwa miaka mingine mitatu zaidi, ili kuhitimisha mpango wake wa kustaafu kazi hiyo akiwa na miaka 70.

Mkwasa: Tulitarajia Kupangwa Na Timu Yoyote
Video: Ridhiwani -Familia ilitikisika nilipohojiwa dawa za kulevya, Makonda aibukia Machinga Complex