Gwiji wa Soka Duniani raia wa Brazil Edson Arantes do Nascimento amethibitisha taarifa za hali yake kuendelea vizuri, baada ya kulazwa kwenye chumba cha uangalizi maalum ‘ICU’ katika Hospitali ya Sao Paulo Albert Einstein.

Pele mwenye umri wa miaka miaka 80, amethibitisha taarifa hizo kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa kwenye chumba cha ICU.

Gwiji huyo ambaye aliwahi kutamba na kikosi cha Brazil na kutwaa ubingwa wa dunia mwaka 1958, 1962 na 1970, pia amewashukuru wanafamilia wote kwa upendo wanaomuonesha na kumfanya kuwa mwenye kutabasamu kila siku.

Pele amekuwa akipatiwa matibabu kwenye hospitali ya Sao Paulo Albert Einstein tangu Agosti 31 mwaka huu, baada ya kugundilika pia ana shida ya upumuaji ambayo kwa sasa imetibiwa.

Azam FC wajipanga kuing'oa Pyramid FC
Simba yaifanyia umafia Young Africans