Jeshi la Misri limeweka wazi picha za kwanza za mabaki ya ndege ya AgyptAir, Flight 804 iliyopotea ghafla angani na kupatikana mapema leo katika habari ya Mediterranean.

Mamlaka za Misri zimeeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa uwepo wa tukio la kigaidi katika kupotea kwa ndege hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka jijini Paris Ufaransa kuelekea jijini Cairo nchini Misri ikiwa na watu 66 wa mataifa mbalimbali, Mei 19 mwaka huu.

Jeshi la Misri limesema kuwa mabaki ya ndege hiyo yamepatikana umbali wa takribani kilometa 290 kaskazini mwa mji wa Alexandria nchini Misri na hakuna mtu yeyote aliyesalimika.

Mabaki 2

Imeelezwa kuwa baadhi ya miili imepatikana ikiwa imeharibika pamoja na vitu vingine kama viti vya ndege pamoja na nguo.

Mabaki 3

Picha za mabaki hayo ziliwekwa kwenye ukurasa wa Facebook wa Jeshi la Misri.

Airtel Yapanga Mikakati Ya Maendeleo Soka La Vijana
Manispaa ya Kinondoni yamuwekea Manji kitanzi kingine ‘Coco Beach’

Comments

comments