Polisi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC eneo la Rubaya Masisi katika jimbo la Kivu kaskazini wanatuhumiwa kuwafyatulia risasi na kuwauwa wachimbaji madini watatu katika mgodi wa Rubaya.

Wakati huo huo watu 100 wengine wamenusurika kifo baada ya kufunikwa na maporomoko ya matope yaliyotokea kwenye eneo la mgodi huo.

Aidha, mkazi mmoja wa wilaya masisi Kivu Kaskazini amesema kuwa baada ya askari hao kufika katika machimbo hayo waliwafyatulia risasi watu hao.

“Baada ya kufika katika mgodi huu, waliwafyatulia risasi watu hao na mmoja alikufa hapo hapo, huku wengine wakifia hospitalini,”amesema raia huyo

Hata hivyo, serikali ya Congo=DRC haijasema lolote kuhusu maafa hayo, lakini Polisi imesema kuwa iliwaona watu hao wakitoka ndani ya mgodi huo huku wakikimbia ndipo ilipohisi wanatoroka madini, ndipo ilipowafyatulia risasi.

Rwanda yadai imeboresha haki za binadamu
Video: Lissu amchambua Dkt. Slaa kama njugu, Msamaha wa babu Seya waibuka Bungeni