Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema limejipanga kuhakikisha Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu na wafuasi wake wanapatiwa ulinzi kwa mujibu wa sheria.

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema askari wake wamejipanga kuuongoza msafara wa kiongozi huyo bila kutaathiri ujenzi wa barabara na ule wa reli ya kisasa unaoendelea kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa, wa Julius Nyerere.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

“Tutampitisha kwenye barabara ambazo ujenzi hauendelei kwa sababu ule ni mradi mkubwa wa
kitaifa tutampitisha kwenye barabara ambazo hazitaathiri masuala ya ujenzi, Polisi tumejipanga kama kawaida tutaendelea na shughuli kuona usalama unaimarika.”

Tundu Lissu, ambaye aligombea urais kupitia CHADEMA mwaka 2020, anatarajia kuwasili nchini hii leo Januari 25, 2023 akitokea nchini Ubelgiji ambako ameishi kwa takribani miaka minne akifanyiwa matibabu.

Ashuhudia jinsi alivyomdhibiti mumewe asichepuke
Phiri, Inonga mambo safi Simba SC