Mwanamuziki Abubakar Katwila maarufu ‘Q Chief’ ameziweka wazi kazi za wasanii wa muziki wa bongo fleva alizozivika taji la ubora kutokana na uhodari wa wasanii husika katika kukamilisha kazi hizo.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram Chilla amemtaja msanii Ali Kiba, Con Boi pamoja na mtayarishaji mahiri wa muziki wa kizazi kipya Marco chali kuwa miongoni mwa wasanii waliukonga moyo wake.

“Nimebahatika kusikiliza few albums za Africa mashariki na kati, sio mbaya nimependa sana album ya Ali Kiba, hongera sana King lakini pia nimebahatika kusikiliza album ya Marco Chali it amaizing i see growth but also niwe muwazi.

Nimebahatika kusikiliza Ep ya mdogo wangu Con Boi, yo it’s amaizing, its real and pure, i see tje future of Hip Hop na najua hii ni kazi kubwa iliyofungwa na waasisi big up to them and now it’s your time Con Boi, we’are here your real funs.” Aliandika.

Q Chief kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao ‘Tonight’ wenye miondoko ya Reggae unaopatuka katika digital platforms zote ikiwamo chaneli yake ya YouTube.

Waziri Ummy aanza na idara ya kinga
Waziri Mkuu awataka mabalozi kuvutia wawekezaji