Rais wa Urusi, Vladimir Putin amekutana na baadhi ya akina mama wa wanajeshi wa Urusi wanaopigana nchini Ukraine, na kusema Serikali ipo pamoja na familia za watoto wao ambao wamepoteza maisha wakiwa vitani.

Putin, amekutana na akima mama hao 17 katika makao yake ya Novo-Ogaryovo, yaliyopo nje ya mji wa Moscow kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya Mama nchini Urusi inayotarajia kufanyika hapo kesho Jumapili ya Novemba 27, 2022.

Baadhi ya akina Mama wa wapiganaji wa Urusi wakiwa katika kikao na Rais Vladimir Putin. Picha ya ABC News.

Akina mama hao, ambao walionesha tabasamu wakati Putin akiingia ukumbini walisikiliza maneno ya ufunguzi ya Putin ingawa hisia zao hazikuoneshwa kwenye ukanda wa video uliotolewa na mpiga picha wa Ikulu.

Warusi wengi wamepelekwa kupigana nchini Ukraine, wakiwemo zaidi ya watu 300,000 waliosajiliwa kama sehemu ya hamasisho lililotangazwa na Rais Putin, mapema mwezi Septemba, 2022.

Serikali yakataa mazungumzo ya amani
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 26, 2022