Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amemteua Ngusa Dismams Samike kuwa Mnikulu Ofisi ya Rais, Ikulu (Comptroller State House – CSH).
Taarifa hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, John Kijazi ambapo amesema kuwa kabla ya uteuzi huo uliofanyika leo Desemba 13, 2016, Ngusa Samike alikuwa akikaimu nafasi hiyo.