Hatimaye leo rais wa zamani wa Brazil, Luiz Inácio Lula da Silva amejisalimisha kwa jeshi la polisi kwa ajili ya kuanza kutumikia kifungo chake cha miaka 12 jela, alichohukumiwa na Mahakama Kuu nchini humo kwa makosa ya rushwa na ufisadi.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 72 amejisalimisha polisi ikiwa amevuka ukomo wa siku alizokuwa amepewa na mahakama kujisalimisha kuanza kutumikia kifungo chake.

Lula alikuwa amejificha kwenye jengo moja maarufu la umoja wa wafanyakazi karibu na mji wa Sao Paulo ambako wafuasi wake walijaa nje wakipinga hukumu yake.

Wafuasi wake walijaribu kuzuia gari la polisi kutoondoka katika eneo hilo lakini hawakufanikiwa.

Baadaye, alisafirishwa kwa helkopta ya polisi hadi jiji la Curitiba anakoenda kutumikia kifungo chake.

Lula ameendelea kupinga uamuzi wa mahakama akidai kuwa umetokana na shinikizo la kisiasa lakini amesema anatii matakwa ya sheria ya kukamatwa.

Alikuwa na mpango wa kugombea tena urais wa Brazil mwaka huu na tafiti za awali zilionesha ana nafasi kubwa zaidi ya kuwa mshindi dhidi ya waliotangaza nia.

Subirini kwanza JPM atunyooshe- Polepole
Kakobe afunguka kuhusu kuitwa Uhamiaji, 'nimejipanga'

Comments

comments