Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amekosolewa vikali na wadau wa mitandao pale alipomtaka Waziri wa Fedha kutafuta njia ya kutoza kodi mitandoa ya kijamii, ili kuzuia kile alichokiita ni “umbeya” unaoenezwa na mitandao hiyo.

Maafisa wa serikali ya nchi hiyo wamesema kuwa wamejadiliana kwa kina kuhusu kauli hiyo, hivyo wanafanya juhudi kuanza kutoza kodi kwa data inayotumika kwenye simu kila siku kuanzia July 2018.

Aidha, Serikali ya Uganda imesema kuwa matumizi ya intaneti katika simu yameongezeka kwa asilimia 15 mwaka uliopita wakati watu wengi zaidi wamekuwa wakitumia huduma za mitandao kwa ajili ya huduma hiyo na kufanya malipo.

“Nafikiri siku hizi, kwa hakika kuna idadi kubwa ya wafanyabiashara ambao wanatumia tu mtandao wa Instagram na Whats App na njia mbali mbali ambazo wanajitangaza kupitia intaneti, Kwa hiyo nafikiri tathmini ya rais ilikuwa haitendei haki malengo ya wale wanaotumia mitandao hiyo,”amesema Blogger Godiva Akullo

Hata hivyo, Maafisa wa Baraza la Mawaziri wanatetea mapendekezo hayo ya kodi, kwamba itasaidia kuboresha miundombinu ya mawasiliano ya simu.

 

Video: BASATA wafunguka kuhusu kufungiwa kwa wasanii
TMA yatoa tahadhari kwa baadhi ya maeneo nchini