Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kushirikiana na sekretarieti ya Baraza la Taifa la Biashara, kuhakikisha mabaraza katika ngazi hiyo yanafanya kazi.

Akizungumza katika Mkutano wa 12 wa Baraza hilo, Rais, Samia amesema kuwa ufanisi wa Baraza hilo unategemea mabaraza hayo ya Mikoa na Wilaya.

Aidha, Rais Samia amejitolea kuwa mlezi wa majukwaa ya wanawake wafanyabiashara na kuwaasa Wakuu hao pia kuendelea kusimamia majukwaa hayo.

“Lengo ni lilelile ikiwa women empowernment (kuwainua wanawake), kama mnavyojua nimejicomit kuwa champion wa suala la economic right na economic justice duniani kwa hiyo mimi nabeba ajenda ya Africa kwenye eneo hilo,” amesema Rais Samia.

Maeneo mengine ambayo Rais Samia ameyaainisha kuwa serikali itayatilia mkazo ni pamoja na eneo la utalii na kuangalia sheria ya TASAF upya.

Baraza hilo limetimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake kwa lengo la kutumika kuwa jukwaa rasmi la majadiliano kati ya serikali na sekta binafsi ili kuwezesha kupatikana kwa maboresho ya sheria, kanuni na taratibu za biashara.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Juni 27, 2021
Bandari ya Bagamoyo kufufuliwa